Loading...
Hali ya majonzi imetanda katika familia moja iliyopo nchini Kenya kaunti ya Kitui baada ya mtoto wao mwenye umri wa miaka 13 kuzamishwa na maji katika bwawa la kuogelea hotelini.
Kijana huyo aliyeandamana na wazazi wake kwenda kusherehekea sikukuu ya krismasi katika hoteli ya Lavanella, kumbe masikini kifo kilikuwa kinatembea naye.
Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Anthony Kamitu alieleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo halisi cha kifo cha kijana huyo.
Familia ya marehemu iliulaumu ongozi wa hoteli kwa kukosa mbinu za kuzuia vifo kama hivyo.
"Hatuelewi kijana wetu alifariki vipi maana alikuwa akiogelea na wenzanke. Bwawa hili lilikuwa limejaa. Usimamizi wa hoteli ulipaswa kuwa na anayesimamia bwawa hilo," baba wa marehemu alisimulia kwa majonzi.
Mwili wa marehemu ulitolewa katika bwawa hilo na kusafirishwa hadi chumba cha kuhifadhia maiti cha Kitui.
Na Khamisi Daudi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SWIMMING POOL ILIVYOTIA DOA KISMASI HUKO KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
12/27/2018 03:41:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/27/2018 03:41:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: