Loading...

MAMBO MAKUU MAWILI JINSI YA KUACHANA NA MCHEPUKO

Loading...
Mchepuko ni mwanamke/mwanaume wa pembeni yaani mbadala wa njia kuu (mke au mpenzi wako). Sasa leo hii tutaangazia ni namna gani tunaweza kuepukana na hawala au kimada kama wahenga wanavyowaita ili ibaki katika penzi la uaminifu.

Kuna mambo makuu mawili kama tutayazingatia vizuri, basi hayo mahusiano ya pembeni yatavunjika kabisa na kubaki salama. Mambo yenyewe ni:-

1. Kumsimulia mchepuko wako mambo mengi mazuri ambayo huwa unafanya uwapo na njia kuu. Kama hiyo haitoshi msimulie mchepuko  kuhusu uzuri wa njia kuu pasipo kuona aibu wala kukosoa uzuri na ubaya wa njia kuu. Kufanya hivyo itamsaidia mchepuko huyo ajisikie vibaya kwani michepuko mingi huwa haipendi kusikia habari zinazohusu njia kuu.

2. Punguza mawasiliano na Mchepuko. Nafahamu fika wakati unapoanza mahusiano na huyo ambaye unamuita after baby mawasilino yalikua ni mazuri sana. Vivyo hivyo kama unataka kuachana na mchepuko  wako basi unatakiwa kufanya ni kufanya kinyume chake, yaani mawasilino yawe ni finyu ikiwezekana yafe kabisa. Muda mwingine akikupigia simu ona kama umeona moto unaowaka.

Kwakuwa mchepuko na chanzo kikubwa cha familia nyingi kupoteza muelekeo na hata ndoa kuvunjika basi kwa kuzingatia mambo hayo mawili utaweza kuokoa ndoa yako. Natumai wote tutabaki njia kuu.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAMBO MAKUU MAWILI JINSI YA KUACHANA NA MCHEPUKO MAMBO MAKUU MAWILI JINSI YA KUACHANA NA MCHEPUKO Reviewed by By News Reporter on 12/26/2018 09:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.