Loading...
Mkuu wa usalama wa eneo la Noida nchini India amesema Waislamu wa eneo hilo hawaruhusiwi kuswali swala ya Ijumaa katika maeneo ya wazi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchini humo taarifa iliyotolewa na mkuu wa usalama wa mji wa Noida amesema waislamu hawaruhusiwi kuswali swala ya Ijumaa katika maeneo ya wazi kama vile bustani za mji.
Katika taarifa hiyo imesema wafanyakazi waisalmu wakiendelea kuswali katika maeneo ya wazi, watakaochukuliwa hatua ni waajiri wao. Taarifa hiyo ilisema kwamba waajiri inapaswa wawaelekeze wafanyakazi waislamu waswali maeneo yaliyoungwa kama msikiti au ofisi.
Inahofiwa kwamba hali ya kuswali swala ya Ijumaa kwa jamaa maeneo ya wazi katika mji wa Noida inaweza ikaenea maeneo mengine isipozibitiwa.
Kutokana na mahakama kuu nchini humo kuwakataza waislamu wanaotoka nje ya mji kuswali swala ya ijumaa katika msikiti uliopo kwenye kaburi la Taj Mahal, Mamlaka ya utafiti wa Archeolojia ya India imepiga marufuku kuswali swala za kawaida pia katika eneo la Taj Mahal.
Na Mohamedi Makame.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WAISLAMU NCHINI INDIA WAPEWA ONYO KUSWALI MAENEO YA WAZI
Reviewed by By News Reporter
on
12/26/2018 09:16:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/26/2018 09:16:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: