Loading...

WATU 50 WAFARIKI PAPO KATIKA AJALI CONGO

Loading...
DRC. Watu 50 wamefariki katika ajali ya barabarani iliyohusisha Basi la abiria na lori nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ndani vya nchi hio ajali hiyo imetokea katika mji wa Kisantu ulio umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu Kinshasa. Lori liliokuwa likielekea eneo la Matadi liligongana na Basi la abiria uso kwa uso. 

Katika ajali hiyo watu 50 walipoteza maisha  na wengine wengi kujeruhiwa. Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali mbalimbali zilizopo mjini Kinshasa.

Mnamo mwezi Oktoba ajali iliyotokea karibu na eneo la Kisantu ilisababisha vifo vya watu 53.
Na Yohana Daudi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WATU 50 WAFARIKI PAPO KATIKA AJALI CONGO WATU 50 WAFARIKI PAPO KATIKA AJALI CONGO Reviewed by By News Reporter on 12/26/2018 09:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.