Loading...
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko wataendelea kusota rumande hadi Januari 3, 2019 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kesi yao.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo akisaidia na wakili Salim Msemo amedai leo Ijumaa Desemba 21, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo, wakili Faraja Mangula amedai kuwa wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, 2019.
Akijibu hoja hiyo, wakili Simon amedai wanaiachia mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa na hakimu Mashauri kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, 2019.
Mbowe na Matiko wako gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali.
Na Hussein Bashe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MBOWE NA MATIKO WAENDELEA KUSOTA RUMANDE, KESI YAO YAHAIRISHWA HADI JANUARI 3 MWAKA 2019
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 04:05:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 04:05:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: