Loading...

MTOTO WA WAZIRI MKUU WA IZRAEL AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK YAFUNGWA KWA UBAGUZI

Loading...
Mtandao wa Facebook umechukua hatua ya kuifungia ukurasa wa mtoto wa Waziri Mkuu wa Izraeli, Benjamini Netanyahu, anyeitwa Yair baada ya kuweka ujumbe ambao hapo awali ulifungiwa ulio wataka "Waislamu wote kuondoka" Izraeli.

Katika ujumbe huo uliowekwa siku ya Alhamisi katika ukurasa wake ya facebook, ni baada ya kutokea mashambulizi ambapo angalau Wapalestina 5 na Waizrael 3, wakiwamo wanajeshi wawili, waliouawa kipindi cha karibuni, Yair Netanyahu aliitisha kuondoka kwa Wapalestina.

"Mnajua wapi kusipokuwa na mashambulizi? Iceland na Japan ambapo hakuna waislamu kabisa," Mtoto huyo wa Waziri Mkuu aliandika.

Katika ujumbe wake mwingine, aliandika kwamba kuna aina mbili tu za suluhu kufikia amani, ni "Wayahudi wote [Izraeli] waondoke au Waislamu wote waondoke".

"Napendekeza chaguo la pili," aliongezea mtoto huyo mwenye umri wa miaka 27.

Facebook ilifuta ujumbe wake huo kwa madai kuwa analipa kisasi kwa kwa kuuliwa wanajeshi wa Izraeli na kunasababisha chuki za kidini.

Ndipo Yair alipoamua kuchukua ujumbe wake uliozuiwa na facebook na kuuweka kama picha katika ukurasa wake wa twitter ili kuukosoa mtandao wa facebook, na baadae masaa 24 mtandao huo mkubwa dunia ulichukua hatua ya kuifuta akaunti yake.
Na Nassir Juma.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MTOTO WA WAZIRI MKUU WA IZRAEL AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK YAFUNGWA KWA UBAGUZI MTOTO WA WAZIRI MKUU WA IZRAEL AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK YAFUNGWA KWA UBAGUZI Reviewed by By News Reporter on 12/17/2018 03:55:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.