Loading...
Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amelazwa katika hospitali moja nchini Ujerumani baada ya hali yake ya afya kuzorota
Dimpoz yuko na tatizo kwenye koo ambalo lilipelekea kufanyiwa upasuaji kule Afrika Kusini miezi minne iliyopita.
Habari za Dimpoz kusafiri hadi Ujerumani zilitangazwa na babake akiwa kwenye mahojiano na wanahabari wa gazeti la Wikienda.
"Niliarifiwa kwamba hali ya afya ya mwanangu ilikuwa inazidi kuzorota, wamempeleka Ujerumani kwa matibabu zaidi na huenda akafanyiwa upasuaji mwingine," Babake Dimpoz alisema.
Meneja wa mwanamuziki huyu Sevens Mosha pia alidhibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Dimpoz anaendelea kupata matibabu na atarejea nyumbani akipata nafuu.
Aidha, wafuasi wake wamemtakia afueni ya haraka kupitia kwenye jumbe mitandaoni.
Haya yanajiri takriban miezi minne tu baada ya mwanamuziki huyo kufanyiwa upasuaji kwenye koo lake nchini Afrika Kusini.
Na Richard Yohana.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

OMMY DIMPOZ AZIDIWA APEREKWA UJERUMANI KWA MATIBABU
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 09:26:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 09:26:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: