Loading...
Maradhi ya zinaa yasiyo ya kawaida yameenea katika kaunti ya Migori huku wenyeji wakilalamikia hatari yake.
Licha ya wataalamu wa afya kukosa kuthibitisha kuhusu ripoti hiyo, wenyeji wa kaunti hiyo wametahadharishwa huku watu watano wakidaiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo uliobatizwa jina Jakadala.
Mwanachama wa bodi ya afya katika serikali ya kaunti ya Migori Isca Oluoch amewatahadharisha wenyeji kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.
Tofauti na maradhi mengine ya zinaa, inadaiwa kuwa jakadala ni hatari zaidi huku ikidaiwa kula na kumaliza sehemu nyeti na hata kusababisha kifo upesi.
Visa vya maradhi hayo yameripotiwa maeneo ya Suna, Nyatike, migodi ya Nyarombo na migodi ya Komito katika kaunti ndogo ya Rongo.
Uvumu kuhusu ugonjwa huo wa zinaa ulienea baada ya mwathiriwa kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Migori. Jamaa huyo amekuwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miaka mitano.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

'JAKADALA' GONJWA JIPYA LA ZINAA LAIBUKIA KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 07:08:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 07:08:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: