Loading...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatano, Desemba 19 alimponda hadharani mshindi wa tuzo za urembo barani Afrika Quiin Abenakyo kwa kutumia nywele bandia za kigeni badala ya nywele zake halisi.
Museveni alimwambia binti huyo kuwa hapendi nywele za kigeni kama alizokuwa ametumia Abenakyo ambazo zilikuwa za Kihindi na kumkata kuziondoa na kutumia nywele zake halisi.
Museveni alidai kuwa Abenakyo aliyeibuka kuwa binti mrembo zaidi barani Afrika alikuwa mrembo lakini nywele zake tu ndizo zilitia dosari urembo wake wa Afrika kwakuwa alitumia nywele za wa Asia.
"Abenakyo ni msichana wa Musoga aliye mrefu na mrembo. Tatizo langu tu ni kuwa alikuwa amevaa nywele za Kihindi. Ninamshauri kuweka nywele zake halisi za Kiafrika. Lazima tuonyeshe urembo wa Kiafrika katika hali yake halisi," Museveni aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Abenakyo alikuwa amemtembelea Museveni kwenye ikulu ya nchi hiyo jijini Entebbe ambayo alifanya mazungumzo na rais huyo.
Abenakyo alikuwa ametoka nchini Uchina baada ya kuhudhuria mashindano ya 68 za binti mrembo zaidi duniani ambapo aliipa nchi yake umaarufu baada ya kumaliza wa pili.
Mwezi Agosti 2018, Abenakyo alituzwa kuwa binti mrembo zaidi nchini Uganda katika mwaka wa 2018/2019.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

RAIS MUSEVENI AMPONDA MISS WORLD AFRIKA, ADAI SIO MWAFRIKA HALISI
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 08:38:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 08:38:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: