Loading...
Klabu ya Manchester United leo imefikia maamuzi ya kumtangaza kocha wao mpya wa muda atakayemrithi kocha Jose Mourinho katika klabu hiyo, uamuzi huo unatangazwa leo ikiwa ni siku moja imepita toka club ya Man United itangaze kusitisha ajira ya Jose Mourinho ndani ya Old Trafford.
Man United leo imemtangaza mchezaji wao wa zamani raia wa Norway, Ole Gunnar Solskjaer kuwa ndio kocha wao mpya atakayemrithi Jose Mourinho hadi mwisho wa msimu wa 2018/2019 hadi watakapotangaza kocha mpya wa kudumu, Ole Gunnar Solskjaer atakuwa kocha wa Man United akishirikiana na Mike Phelan na Michael Carrick na Kieran McKenna.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ole Gunnar Solskjaer aliyetangazwa kuwa kocha wa muda wa Man United, aliwahi kuwa mchezaji wa zamani wa Man United kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2007 na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Norway, Solskjaer kabla ya kujiunga na Man United kama kocha wa muda alikuwa akiifundisha Molde na amewahi kuifundisha Cardiff City na timu ya Man United ya wachezaji wa akiba.
Na Frank Cosmas.

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAN U WATANGAZA RASMI MBADALA WA MOURINHO
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 01:57:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/19/2018 01:57:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: