Loading...

RAIS PUTIN WA URUSI ATAKA MUZIKI WA RAP (KUFOKA) UDHIBITIWE

Loading...
Kufuatia kukua kwa muziki wa kufoka maarufu kama Rap/HipHop kwa vijana wa Urusi, Rais Vladimir Putin amawataka viongozi wa mamlaka za utamaduni  kushauri kwa maana ya kudhibiti muziki maarufu wa kufoka na sio kuufungia.

Putin alisema "Kama ni ngumu kuuzuia, basi tuutawale na kutoa muelekeo wake."

Lakini Putin akiyasema hayo katika mkutano uliofanyika St. Petersburg na washauri wa maswala ya utamaduni siku ya Jumamosi kuwa kujaribu kufungia wasanii kutumbuiza majukwaani kunasababisha kushusha umaarufu wao.

Putin alinukuu kwamba "Muziki wa kufoka unasimamia katika nguzo tatu, madawa ya kulevya, ngono na harakati." Lakini anaangalia zaidi swala la madawa ya kulevya, alisema "Hii ni njia ya kushushia hadhi taifa letu."

Alisema "Propaganda ya madawa ya kulevya ni mbaya zaidi kuliko lugha chafu"
Na Frank Zabron.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS PUTIN WA URUSI ATAKA MUZIKI WA RAP (KUFOKA) UDHIBITIWE RAIS PUTIN WA URUSI ATAKA MUZIKI WA RAP (KUFOKA) UDHIBITIWE Reviewed by By News Reporter on 12/17/2018 10:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.