Loading...

TAHADHARI: MVUA YA SIKU 5 NA MAFURIKO KUTARAJIWA, MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA YATAJWA

Loading...
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini humo kutokana na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo.

Hayo yameelezwa siku ya Jumapili Desemba 16, 2018 kati  taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mamlaka hiyo.

TMA imewataka wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhali hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kuanzia leo Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Desemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mafuriko jambo ambalo litafanya baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

“Hii inamaanisha kuwa mafuriko yatatokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi,” inaeleza.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAHADHARI: MVUA YA SIKU 5 NA MAFURIKO KUTARAJIWA, MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA YATAJWA TAHADHARI: MVUA YA SIKU 5 NA MAFURIKO KUTARAJIWA, MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA YATAJWA Reviewed by By News Reporter on 12/17/2018 09:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.