Loading...

BASATA KUTOA ADHABU KALI KWA DIAMOND NA RAYVANNY KUTUMBUIZA 'NYEGEZI' TAMASHA LA WASAFI

Loading...
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema neno kwa kitendo Wasanii wa Bongo fleva Diamond Platinumz na Rayvanny kutumbuiza wimbo wao wa 'Mwanza' ambao umefungiwa.

Mwezi uliopita BASATA walitangaza kuufungia rasmi wimbo wa 'Mwanza' kwa madai kuwa wasanii hao wamekiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maudhui ya wimbo huo.

Diamond na Rayvanny kwa pamoja waliutumbuiza wimbo huo siku ya Jumamosi, tarehe 15 Disemba, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza, huku maelfu ya mashabiki wakishangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba.

Katibu Mtendaji wa Baraza Ndug. Godfrey Mngereza katika mahojiana na mtandao mmoja wa habari hapa nchini alifunga kwamba msanii Diamond ameonyesha dharau kwa kiwango cha juu, na yupo kikazi Arusha ila ameshawasiliana na Mwenyekiti wa baraza na BASATA itakuja na majibu muafaka kuhusu hili swala kwakuwa ameshapata taarifa.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BASATA KUTOA ADHABU KALI KWA DIAMOND NA RAYVANNY KUTUMBUIZA 'NYEGEZI' TAMASHA LA WASAFI BASATA KUTOA ADHABU KALI KWA DIAMOND NA RAYVANNY KUTUMBUIZA 'NYEGEZI' TAMASHA LA WASAFI Reviewed by By News Reporter on 12/17/2018 08:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.