Loading...
Mwanamuziki maarufu na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi anayefahamika kwa jina la Bobi Wine ameamua kukimbilia mafichoni baada ya kutafutwa na polisi ya Uganda katika hoteli alipokuwa anaishi, wakili wake amesema.
Bobi Wine alitarajiwa kufanya tamasha la muziki siku ya Jumamosi katika mji wa Jinja, kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala, wakati polisi iliendesha msako katika hoteli yake.
Bobi Wine "alilazimika kukimbilia mafichoni," huku ndugu zake na marafiki zake wa karibu wakikamatwa na kupigwa, amesema Robert Amsterdam, mwanasheria wa Bobi Wine mwenye makazi yake mjini London.
"Polisi walivamia hoteli ambapo tulikuwa tumepumzika kabla ya tamasha la usiku wa leo na kuwatia mbaroni baadhi ya wajumbe wa timu yetu. wakati huu tunapoongea, polisi imezingira eneo lote kwa kunisaka, "Bobi Wine ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Mwanasheria wa nyota huyo maarufu wa kizazi kipya ametaja operesheni hiyo ya polisi kama "kitendo cha aibu cha ukandamizaji wa kisiasa kinachofanywa na serikali ya Uganda kwa kukiuka haki za binadamu za Bobi Wine".
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MWANAMUZIKI BOBI WINE AKIMBILIA MAFICHONI BAADA YA MSAKO MKALI
Reviewed by By News Reporter
on
12/17/2018 08:26:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/17/2018 08:26:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: