Loading...
Mamilioni ya Wakristo ulimwenguni kote tarehe 25 Disemba, kila mwaka husherehekea Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu, lakini karne kadha zilizopita baadhi ya Wakristo walipiga marufuku kusherehekea siku hii muhimu kwenye kalenda.
Tukianza na Uingereza, miaka ya nyuma jamii ya Waingereza waliona haja ya kuzuia shughuli ambazo waliziona zimekuwa zikienda kinyume na mafundisho ya Kikristo.
Mambo kama Kunywa pombe kupita kiasi, mkusanyiko wa watu wengi wanaopiga kelele za shangwe, biashara kufungwa mapema, familia na marafiki kujumuika pamoja kwa ajili ya chakula maalum cha sikukuu, nyumba kupambwa kwa miti na hata mitaani nyimbo za Krismasi kutawala.
Hivyo vitu vilionekana ni dhambi ni sawa na kumkufuru Mungu, ila vyote vilifanyika siku maalumu ambayo waliita KRISMASI.
CHAZO HASA CHA KUFUNGIA SIKUKUU YA KRISMASI
MWAKA 1644, Wakristo waliojulikana kama Puritans, ambayo walidai wao ndiyo 'Wakristo wa Kweli' wao ndiyo walinuia kabisa kuifuta sikukuu hiyo na sheria za kuizuia zikatungwa.
Huku wakiamini kwamba hakukuwa na mahali popote kwenye Biblia ambapo ilikuwa imeandikwa au kudokezwa kwamba Yesu Kristo alizaliwa 25 Desemba.
Marufuku hayo yaliendelea mpaka makundi ya watu (waliodaiwa ni wapagani) walipoanza kuandamana wakidai kurudishwa kwa Krismasi yao. Ilipofika miaka ya 1660 kipindi cha utawala wa Mfalme Charles wa pili ndipo sikukuu ya krismasi ikarudishwa tena.
KUFUNGIWA MAREKANI
MWAKA 1659 hadi 1681, katika jimbo la Massachusetts, Marekani hawakuwa na Krismasi. Na pia walipiga marufuku sherehe hizo wakiwa na sababu zinazofanana na za Uingereza. Kwa kuwa huko napo walipatikana waumini wa Puritan.
JE! SABABU ZAO ZILIKUWA NA MASHIKO KIBIBLIA?
Bado hakujakuwa na maafikiano kuhusu ni lini hasa Yesu alizaliwa.
Wataalam wa dini wanafikiri kwamba labda yalikuwa majira ya kuchipua kwa sababu kuna taarifa za wachungaji walikiwa nyikani wakiwachunga kondoo wao.
Ingekuwa Desemba, ambapo huwa msimu wa baridi, basi wasingekuwa malishoni, wangekuwa wametafuta hifadhi maeneo yenye joto.
Au pengine yalikuwa majira ya kupuputika kwa majani. Kuna uwezekano kwamba wachungaji walikuwa wanawaangalia kondoo wao msimu wao wa kupandana ili kuwatenganisha kondoo jike ambao tayari walikuwa wamepandwa na kutungishwa mbegu.
Biblia haijatoa tarehe yoyote.
NA Petro Phillipe.

SABABU YA KRISMASI KUPIGWA MARUFUKU UINGEREZA NA MAREKANI MIAKA YA NYUMA
Reviewed by By News Reporter
on
12/26/2018 01:54:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/26/2018 01:54:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: