Loading...
Mamlaka za uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) imetangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa umepangiwa kufanyika Jumapili kwa wiki moja.
Uchaguzi huo sasa umepangiwa kufanyika Jumapili tarehe 30 Desemba badala ya tarehe 23 Desemba.
Tume hiyo imesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuchelewa kwa shughuli ya kufikisha vifaa na mitambo ya kupigia kura vituoni.
Uchaguzi wa DRC umekuwa ukisogezwa mbele kwa zaidi ya miaka miwili sasa, huku rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila akishutumiwa kwa kutoa visingizio kadhaa vya kuahirisha uchaguzi ili aendelee kusalia madarakani.
Wiki iliyopita ghala la tume ya uchaguzi liliopo jijini Kinshasa liliteketea kwa moto na kuunguza baadhi ya vifaa muhimu vya uchaguzi, hata hivyo, mamlaka ziliwahakikishia wananchi kuwa moto huo hautaathiri kufanyika kwa uchaguzi.
Tangazo hilo la ghafla linatokea wakati polisi walimzuia mmoja wapo wa wagombea wakuu wa upinzani wa kiti cha urais Martin Fayulu kuzindua kampeni zake katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SAKATA LA UCHAGUZI DRC: MAMLAKA YATANGAZA KUHAIRISHA UCHAGUZI
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 09:37:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/21/2018 09:37:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: