Loading...

SERENGETI BOYS KUBEBA KOMBE BOTSWANA LEO?

Loading...
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), inatarajia kushuka dimbani Botswana leo kucheza mechi ya fainali dhidi ya kisiki kilichoishinda awali, Angola, kuwania ubingwa wa michuano ya Kanda ya Tano kwa Vijana 'Region 5 Youth Games Boys Compitition Botswana 2018'.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kwa Serengeti Boys, kufuatia kuchezea kichapo cha mabao 2-0 zilipokutana awali katika michuano hiyo inayofanyika Botswana mwaka huu.

Baada ya kuchezea kichapo hicho kutoka kwa Angola, Serengeti Boys ilizidi kuimarika na kushinda mechi zote tatu za mwisho hivyo kutinga fainali.

Serengeti iliichapa Malawi U-17 2-1 kisha ikaitandika Afrika Kusini U-17 mabao 2-0 kabla ya kuitoa Zambia kwa mikwaju ya penalti 5-4 katika mechi ya nusu fainali kufuatia kutoka sare ya bao 1-1.

Kikosi hicho kilichopo chini ya Kocha Oscar Milambo, kitakuwa na fursa ya kulipa kisasi leo na kurudi na kombe hilo.
Na Hussein Bhaji.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SERENGETI BOYS KUBEBA KOMBE BOTSWANA LEO? SERENGETI BOYS KUBEBA KOMBE BOTSWANA LEO? Reviewed by By News Reporter on 12/16/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.