Loading...

GANDA LA RISASI ILIYOMUUA MKWAWA YABAINIKA, NI UTHIBITISHO KUWA ALIJIUA

Loading...
WATAFITI wa mambo ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamethibitisha kupatikana kwa ganda la risasi la bunduki aliyoitumia Chifu wa Wahehe, Mtwa Mkwawa kujiua.

Ganda hilo limepatikana kwenye eneo la Mlambalasi, Kalenga  alikokuwa ameweka maficho yake wakati akipigana vita vya msituni dhidi ya Wajerumani zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Akitangaza rasmi jana ugunduzi huo, mmoja wa watafiti hao, Dk. Frank Masele, alisema ugunduzi wa risasi hiyo ya bunduki aina ya Mauser iliyotengenezwa  Ujerumani mwaka 1871, unathibitisha kuwa Mkwawa alijiua kwa kutumia silaha hiyo.

Taarifa ya utafiti huo ilitolewa katika kongamano la Maonyesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayoendelea mjini hapa huku watafiti wa Chuo Kikuu cha Iringa wakitangaza maeneo mapya matatu ya vivutio vya utalii yaliyotumika kuchimba na kufua chuma wakati wa vita vya Mkwawa dhidi ya wajerumani. Chuma hicho kinadhaniwa kilitumika kufua silaha zilizotumika na jeshi la Mkwawa.

Silaha hiyo ni moja ya zaidi ya 300 alizoziteka kwenye vita iliyogharimu maisha ya zaidi ya askari 300 wa Ujerumani akiwamo kamanda wao, Emil von Zelewski, mwaka 1891.

Dk. Masele alisema hatua hiyo inadhihirisha ukweli dhamira ya Mkwawa kujiua ulikuwa wazi na ushahidi upo, hivyo watu wakitaka kuuona watembelee Kalenga ambako kumehifadhiwa fuvu lake. Alisema fuvu hilo lina tobo katikati.
Na George Mabula.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
GANDA LA RISASI ILIYOMUUA MKWAWA YABAINIKA, NI UTHIBITISHO KUWA ALIJIUA GANDA LA RISASI ILIYOMUUA MKWAWA YABAINIKA, NI UTHIBITISHO KUWA ALIJIUA Reviewed by By News Reporter on 12/16/2018 08:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.