Loading...

ALICHOSEMA KAMANDA SHANNA JUU YA KUTEKWA KWA SHEIKH MWANZA

Loading...
Baada ya taarifa za kutekwa kwa Mwalimu Mkuu wa kitengo cha Dini shule ya Sekondari Islamiya Sheikh Bashiru Habibu kuzagaa kila kona, Kamanda wa Polisi Mwanza Jonathan Shanna alijitokeza kwa umma ili kutoa ufafanuzi.

Kamanda Shanna amesema:

"Sheikh aliondoka na Kijana akiwa anamsindikiza ili akaonane na Baba wa Kijana huyo, alipofika nje ya Chuo aliingia ndani ya gari na wenzake walidhani anaondoka anaenda sehemu fulani, baada ya kuingia ndani ya gari hakurudi"

Aliongezea: "Jeshi la Polisi linaendelea kufanya ufuatiliaji wa kina kujua nani waliokuja kumchukua, na tunataka kujua nani waliondoka nae, tunataka kujua walikwenda nae wapi na pia tunaendelea kuchunguza yupo wapi na anafanya nini?. Niwaombe kuwa Jeshi la Polisi linafanya ufuatiliaji wa kina na nina amini ndani ya muda mfupi tutampata kwa sababu tunazo nyenzo za kutosha na tunao uwezo mkubwa"
Na Jackline Mercy.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ALICHOSEMA KAMANDA SHANNA JUU YA KUTEKWA KWA SHEIKH MWANZA ALICHOSEMA KAMANDA SHANNA JUU YA KUTEKWA KWA SHEIKH MWANZA Reviewed by By News Reporter on 12/16/2018 08:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.