Loading...
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge ukikamilika utakuwa mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki kwa kuzalisha megawati 2,115.
Akizungumza leo Jumatano Desemba 12, 2018 Ikulu Dar es Salaam wakati wa utiaji saini wa ujenzi wa mradi huo katika Bonde la Mto Rufiji mkoani Pwani, Dk Kalemani amesema bwawa linalofuata kwa kuzalisha umeme mwingi ni la Bujagari nchini Uganda, likitarajiwa kuzalisha megawati 300 tu.
"Afrika Mashariki sasa ni wa kwanza tukiwa na megawati 2,115. Bwawa lililokuwa likiongoza kabla yetu ni lile la Bujagari la Uganda bado linajengwa na lina megawati 300," amesema Dk Kalemani.
Amesema kwa Afrika, Tanzania itakuwa ya nne na kwamba nchi inayoongoza kwa kuwa na mabwawa makubwa ni Ethiopia, akibainisha kuwa bwawa lake la Renaissance linaloendelea kujengwa litazalisha megawati 6,450 na ujenzi wake utakamilika 2022.
Na Francis Ngule.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

TANZANIA KUONGOZA KUZALISHA UMEME AFRIKA MASHARIKI, AFRIKA KUSHIKA NAFASI YA NNE
Reviewed by By News Reporter
on
12/12/2018 04:50:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/12/2018 04:50:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: