Loading...

UCHAGUZI DRC: MAJIMBO MAWILI YAHAIRISHIWA UPIGAJI KURA

Loading...
Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetangaza Jumatano kuwa imeahirisha uchaguzi wa Disemba 30 kwenye maeneo kadhaa nchini humo hadi  mwezi Machi mwakani kutokana na mlipuko wa Ebola na mapigano.

Upigaji kura katika uchaguzi unaopangwa kufanyika  disemba 30 tayari ulishaahirishwa kwa wiki moja baada ya tume kusema moto uliozuka kwenye ghala la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi mjini Kinshasa ulitatiza uwezekano wa zoezi hilo kuendelea.

Kulingana na tume hiyo ucheleweshaji huo wa uchaguzi kwenye maeneo hayo hautathiri ratiba ya uchaguzi wa  rais ambao unafanyika kwa pamoja na uchaguzi wa bunge na majimbo.

Kwa mujibu wa CENI Matokeo ya uchaguzi wa rais yatatangazwa Januari 15 na rais mteule ataapishwa Januari 18 mwaka 2019.

Hata hivyo tume hiyo haikutoa maelezo yoyote juu ya ni vipi matokeo ya kura ya urais yatajumuishwa  na yale ya majimbo ambayo hayatapiga kura Jumapili ijayo ambayo uchaguzi umepangwa miezi miwili baada ya rais mpya kuapishwa.
Na Saleh Jabir.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UCHAGUZI DRC: MAJIMBO MAWILI YAHAIRISHIWA UPIGAJI KURA UCHAGUZI DRC: MAJIMBO MAWILI YAHAIRISHIWA UPIGAJI KURA Reviewed by By News Reporter on 12/27/2018 10:15:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.