Loading...
Miongoni mwa waliokumbana na zahama hiyo ni pamoja na waliokuwa vigogo wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwamo Mkurugenzi wake Mkuu, Nehemia Mchechu, ambaye tangu aingie katika uongozi wa shirika hilo, alijipatia sifa kemkem kutokana na maendeleo ya shirika hilo.
Machi, mwaka huu, Mchechu alijikuta akipoteza kazi na Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo , Blandina Nyoni, baada ya Rais Magufuli kutofurahia mwenendo wa hali ilivyokuwa ikiendelea ndani ya NHC.
Aprili 6 mwaka huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Maje, kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Tumbuatumbua hiyo iliendelea kutikisa baada ya Septemba 6, mwaka huu, Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola na kumteua Kamishna wa Polisi mwingine Diwani Athumani kushika nafasi hiyo. Diwani alitokea Kagera ambako alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo.
Aidha. Novemba 8, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumrejesha nchini aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Alphayo Japani Kidata na alimwondolea hadhi ya ubalozi.
Kigogo mwingine alionja shubiri ni aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza Juma Malewa, ambaye alitimuliwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, Julai 5, baada ya kuchelewa kwenye kikao alichoitisha baina yake na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Oktoba 31 mwaka huu, mfanyabiashara mashuhuri na ndugu wa mfanyabiashara tajiri Rostam Aziz, Akram Aziz alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Novemba 23 mwaka huu, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, walifutiwa dhamana kwenye kesi inayowakabili na wanaendelea kusota mahabusu mpaka kesi yao itakapotajwa tena mwakani.
Pia Novemba, mwaka huu, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, aliyekuwa akishikiliwa na polisi kwa siku tatu kwa mahojiano alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka yanayomkabili.
Januari mwaka huu, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, alikamatwa na kushtakiwa kwa kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi.
Na Chama Ujugu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

VIGOGO WALIOKIONA CHA MTEMA KUNI 2018
Reviewed by By News Reporter
on
12/30/2018 05:48:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/30/2018 05:48:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: