Loading...

WANYARWANDA WAOMBOLEZA KIFO CHA SHUJAA WA MAUAJI YA KIMBARI

Loading...
Raia wa Rwanda wanaomboleza kifo cha Zura Karuhimbi, mama aliyehatarisha maisha yake kwa kuwaficha zaidi ya watu 100 wakati wa mauaji kimbari mwaka 1994.

Ripoti zinasema kuwa, mama huyo mzee alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 93 huku wengine wakisema alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 100.

Kilichowagusa raia wa Rwanda ni kuwa, mama huyo alihakikisha kuwa, watu wengine wanakuwa salama dhidi ya waasi wa Interahamwe licha ya mume wake na watoto wake kuuliwa.

Rais Paul Kagame, aliwahi kumpa tuzo ya heshima kwa kitendo hicho.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANYARWANDA WAOMBOLEZA KIFO CHA SHUJAA WA MAUAJI YA KIMBARI WANYARWANDA WAOMBOLEZA KIFO CHA SHUJAA WA MAUAJI YA KIMBARI Reviewed by By News Reporter on 12/19/2018 11:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.