Loading...

CHANGAMOTO NI FURSA YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA KUFIKIA MALENGO YETU

Loading...
Ukiongea na watu waliofanikiwa katika mambo mbalimbali yakiwemo mafanikio ya kiuchumi utasikia wakieleza magumu na changamoto mbalimbali walizopitia hadi kufikia pale walipo. Ki ukweli hakuna mafanikio ya moja kwa moja yasiyo na changamoto ama vikwazo vya hapa na pale.

Wengi wanabainisha kuwa mafanikio yao 
yamechangiwa na vitu kadhaa ikiwemo uwezo wao wa kujenga mtazamo chanya kila wanapokutana na changamoto yoyote. Kwao changamoto ni fursa ya kujifunza na kubaini namna bora ya kufikia wanachokitaka

Wewe una mtazamo gani dhidi ya changamoto zako? Siri ya kufikia kile ulichokusudia katika maisha ni pamoja na kuwa na mtazamo chanya dhidi ya hali yoyote ile unayokutana nayo, bila kuwa na mtazamo wa kuangalia nini unajifunza kutoka katika changamoto zako utajikuta unakata tamaa na kushindwa kuendelea.

Badala ya kutumia muda mwingi kufikiri matatizo, tumia muda huo kutathimini nini unajifunza katika changamoto unazopitia ili kubaini namna bora ya kusonga mbele kutimiza malengo yako.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
CHANGAMOTO NI FURSA YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA KUFIKIA MALENGO YETU CHANGAMOTO NI FURSA YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA KUFIKIA MALENGO YETU Reviewed by By News Reporter on 1/20/2019 11:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.