Loading...

KENYA: GAIDI KATIKA SHAMBULIO LA DUSTID2 ATAMBULIKA, FAMILIA YAKE YAKAMATWA

Loading...
Maafisa wa upelelezi wanaofanya uchunguzi kuhusiana na shambulio la kigaidi la DustiD2 wameweza kumtambua mshambuliaji aliyejitolea mhanga kwa kujilipua katika eneo la 14 Riverside.

Mahir Khalid Rizik ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 alizaliwa katika kijiji cha Majengo jijini Mombasa. 

Mahir alisomea katika madrassa ya msikiti ya Musa yanayojulikana kwa sifa mbaya hasa za kuendeleza itikadi za kigaidi.

Mshukiwa alisajiliwa katika kikundi cha ugaidi kilichokuwa kikiwahangaisha maafisa wa usalama katika kijiji cha Majengo kabla ya kutorokea nchini Tanzania mwaka wa 2014. 

Imeripotiwa kuwa Mahir hakuishi sana Tanzania kwani alihamia Somalia ambapo alijiunga rasmi na kikundi cha ugaidi cha al- Shabaab mwaka wa 2015.

Gaidi huyu anasemekana alirejea humu nchini kisiri kupita mpaka wa kaunti ya Mandera Jumapili Januari 13, siku mbili tu kabla ya kutekeleza shambulio la Dusit D2. 

Kulingana na shahid mmoja, gaidi huyo alifika katika eneo la 14 Riverside mapema kabla ya magaidi wenzake ili kufahamu vema eneo hilo. 

Kabla ya Mahir kujilipua, alikuwa akiwasiliana na gaidi mkuu Ali Salim Gichunge anayeaminika kupanga shambulio hilo kwa njia ya simu.

Kupitia kwenye kamera ya CCTV, Mahiri anaonekana akiongea kwa simu huku watu wawili wakipita kando yake kabla ya kujilipua. 

Abdulahi Ogelo ambaye alimpita gaidi huyo kabla ya kujilipua aliiambia runinga ya NTV kwamba jamaa huyo alikuwa wakiwauliza wenzake mahali walikokuwa, ishara kwamba alikuwa anawaarifu aanze mashambulizi.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI

Mke na baba mzazi wa Mahir mpaka sasa wapo chini ya ulinzi baada ya kushikiliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi, jeshi la polisi linaamini watu wa karibu wa gaidi huyo ni muhimu sana kwa sasa ili kuweza kufahamu mizunguko yake ya mara mwisho kabla ya kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 21 huku kadhaa wakiachwa na majeraha mabaya ya risasa.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KENYA: GAIDI KATIKA SHAMBULIO LA DUSTID2 ATAMBULIKA, FAMILIA YAKE YAKAMATWA KENYA: GAIDI KATIKA SHAMBULIO LA DUSTID2 ATAMBULIKA, FAMILIA YAKE YAKAMATWA Reviewed by By News Reporter on 1/20/2019 11:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.