Loading...
Mwanamuziki wa Uganda ambaye pia ni bloga Michael Kalinda, almaarufu Ziggy Wine, ameaga dunia kufuatia majeraha aliyoyapata wakati wa tukio la kuteswa.
Mwanachama huyo wa kundi la Firebase Crew alitekwa nyara na watu wasiojulikana alipokuwa njiani kwenda studio kurekodi muzikieneo la Kamwokya, Julai 21 na baadaye kupatikana ametupwa katika Hospitali ya Mulago.
Wakati madaktari wakimchunguza, Ziggy alikuwa amekomoewa macho na vidole vyake viwili vilikuwa pia vimenyofolewa.
Kifo cha mwanamuziki huyo kilitokea Jumapili, Agosti 4 na kuthibitishwa mapema Jumatatu na James Mubiru, aliyekuwa akifanya kazi karibu naye.
“Ni vigumu kuamini kwamba kaka yangu, rafiki yangu na mwenzangu katika mpambano ameaga dunia. Tumejaribu kila tuliloweza kumwokoa Ziggy lakini kwa bahati maya, haikuwezekana,” Mubiru alisema Jumatatu, Agosti 5.
Kulingana na ripoti za New Vision la Uganda, pikipiki aliyokuwa akitumia Ziggy bado haijulikani ilipo.
Hadi kifo chake, mwanamuziki huyo alikuwa akifanya kazi kwa karibu sana na kundi la Firebase Crew linalomilikiwa na Mbunge wa Kyadondo Mashariki na mwanamuziki Robert Kyagulanyi Ssentamu (Bobi Wine).
Mnamo Alhamisi, Agosti 1, Bobi Wine alisema jinsi alivyomwona rafiki yake na kuelezea hali yake.

Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MFUASI MKUBWA WA BOBI WINE AUAWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
8/06/2019 07:41:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: