Loading...
MWENYEKITI Mpya wa Baraza la
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Prof. Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kushikamana katika Umoja na Mshikamano baina yao ili kujenga Uchumi imara na kuleta Maendeleo ya wananchi wake.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Prof. Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kushikamana katika Umoja na Mshikamano baina yao ili kujenga Uchumi imara na kuleta Maendeleo ya wananchi wake.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa nafasi hiyo jana Jijini Dar es Salaam, Prof. Kabudi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, alisema wakati umefika kwa Nchi za SADC kuungana pamoja katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika taasisi mbalimbali za kikanda na kujenga msingi imara wa ushirikiano.
Prof. Kabudi alisema kwa miaka mingi Nchi za SADC zimekuwa na ushirikiano mkubwa baina yao hivyo wakati umefika kwa wananchi wa Mataifa hayo kushuhudia manufaa ya ushirikiano huo yakileta manufaa makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Aliongeza kuwa Tanzania kwa upande wake imeendelea kuwa nchi rafiki na mshirika wa karibu kwa mataifa yote ya SADC kama inavyojidhihirisha katika historia ya mapambano ya uhuru wa Nchi nyingi za Kusini mwa Afrika, ambapo mataifa mbalimbali yaliweka kambi kwa ajili ya wapigania uhuru wake katika harakati zao za kudai uhuru kutoka kwa wakoloni.
“Mwaka huu tunatimiza miaka 20 tangu kufariki wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi shupavu aliyejitoa pamoja na viongozi wengine wa SADC katika kupigania harakati za ukombozi wa Afrika, tunapaswa kumuenzi kwa kuhakikisha tunaimarisha umoja na ushirikiano uliopo kwa maslahi ya wananchi wetu” alisem Prof. Kabudi.
Prof. Kabudi aliwataka Viongozi wa SADC kuimarisha Umoja kwa kuwa ndiyo silaha kubwa ya ushindi katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndani ya Nchi za SADC pamoja na kutoa ushirikiano wa karibu zaidi kwa sekta binafsi kwa ajili ya kuibua na kujenga fursa za uchumi.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
PROF KABUDI: TUENDELEE KUSHIKAMANA KUJENGA JUMUIYA IMARA KWA MASLAHI YA WANANCHI WETU
Reviewed by Distri Music
on
8/14/2019 08:55:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: