Loading...

DJ AUWAWA UGANDA KWA KUCHEZA MIZIKI YA KUUDHI

Loading...
Kizaazaa kilizuka nchini Uganda baada ya wanaburudani kumvamia DJ mmoja na kumuua kwa madai kuwa alikuwa akicheza miziki isiyovutia.

Wanaburudani hao walidai kuwa DJ Jerry Okirwoth alikuwa akicheza miziki mbovu na kila mara wangemuomba awachezee miziki wanayoipenda alikuwa akiwapuuza.

Kulingana na shahidi, DJ huyo alitupiwa matusi kwa kupoteza muda wa wanaburudani hao na pesa zao kwa kucheza muziki za kuudhi.

Ilifahamika kuwa DJ huyo alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Parombo na alikuwa amemshikilia tu DJ mwenzake aliyekuwa mapumzikoni. 

Kufuatia kisa hicho, kamishna wa wilaya wa eneo hilo William Bob Labeja alipiga marufuku disko za usiku hadi mwenye klabu hiyo atakapowahakikishia wafanyakazi wake kwamba kuna usalama wa kutosha.

"Mimi kama mkurugenzi mkuu wa usalama katika wilaya, sitakubali disko lolote kufanyika usiku katika eneo hili, na yule atakayekiuka sheria hii atachukuliwa hatua kali ya kisheria," Labeja alisema.

Labeja pia alisema uchunguzi umeanzishwa ili kuwakamata waliohusika katika kumshambulia DJ huyo na kusababisha kifo chake.
Na Catherine Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DJ AUWAWA UGANDA KWA KUCHEZA MIZIKI YA KUUDHI DJ AUWAWA UGANDA KWA KUCHEZA MIZIKI YA KUUDHI Reviewed by By News Reporter on 1/20/2019 10:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.