Loading...
Wakati magaidi walipovamia hoteli ya DusitD2 eneo la 14 Riverside Drive, Nairobi, Jumanne, Januari 15, maafisa wa usalama wa Kenya walitumwa katika eneo hilo mara moja kuokoa maisha na hawakuwa peke yao.
Inayat Kassam, ambaye ni mwalimu wa masuala ya ulinzi wa Elite Defence Academy (EDA) Krav Maga pia alishiriki shughuli ya uokozi.
Kassam, imefahamika kuwa ni mtaalamu wa mafunzo ya kupambana na visa vya kigaidi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Scorpio Africa Ltd jijini Nairobi, alikuwa mmoja wa maafisa waliofika DusitD2.
Kulingana na Elite Defence Academy (EDA), Kassam pia alikuwapo wakati wa tukio la kigaidi la Westgate 2013 lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 70.
Akiwa kiongozi wa oparesheni, alifanikisha shughuli za uokozi Westgate Mall na alikuwa msaada mkubwa sana katika kuyaokoa maisha ya wengi.
Weledi na uzoefu wake iliwafurahisha Wakenya waliomuona akishirikiana na maafisa wa polisi wa vitengo mbalimbali kuwaokoa majeruhi na watu waliokuwa wametekwa nyara katika jumba hilo.
Zaidi ya watu 700 waliokolewa hai kutoka Dusit, na Rais Uhuru Kenyatta amevipongeza vikosi vya polisi kwa kazi yao nzuri katika kukabiliana na magaidi hao.
Shughuli za uokozi zilianza Jumanne, Saa tisa alasiri mara baada ya magaidi hao kuingia katika ua wa hoteli hiyo ambayo ipo katika jumba la ghorofa saba na zilikamilika Jumatano, Januari 16.
Watu kadhaa waliumia wakati wa uvamizi huo, uliotokea wakati wa maadhimisho ya shambulizi la El Ade lililosababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi 100 wa Kenya nchini Somalia.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

KUTANA NA MSAMARIA ALIYEJITOLEA MAISHA YAKE KUWAOKOA RAIA WEMA SHAMBULIO LA DUSIT2D
Reviewed by By News Reporter
on
1/19/2019 02:40:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: