Loading...

JAMAA APATWA APATWA NA MAKUBWA BAADA YA KUIBA PESA YA RAMBI RAMBI

Loading...
Kenya. Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 33 wa kijiji cha Kakola, Rachuonyo Mashariki, kaunti ya Homabay ambaye alishirikiana na rafikiye kuiba pesa za matanga amefariki.

Inadaiwa kuwa Geoffrey Odhiambo pamoja na rafikiye waliingia nyumbani kwa Peter Agira kulikofanyika matanga Ijumaaa, Januari 18 na kuiba Sh 56,000 pesa za Kenya (sawa na Tsh 1.2/- Milioni), pesa zilizochangwa na waombolezaji wakati wa mazishi.

Baada ya mazishi ya Agira, Onoka anadaiwa kuingia nyumbani humo usiku akisaidiwa na rafikiye hadi wakafanikiwa kuiba hela hizo.

Familia hiyo ilishangaa kukosa pesa walizoweka kwenye chumba maalum keshowe na hapo ndipo walipoamua kutafuta huduma za mganga. 

Kabla ya mganga huyo kuanza kushugulika zake, alitoa tahadhari kwa washukiwa wa wizi akiwashauri kurudisha hela hizo kabla kujipata pabaya.

Jumapili, Januari 20, jamaa ambaye aliomba jina lake libanwe aliizuru boma hiyo na kurudisha mgao aliyoiba. 

Onoka kwa upande wake hakutikiswa licha ya kupata habari kuwa mganga aliwasili kwa ajili ya kumroga. Ili kumuokoa marehemu, mganga huyo aliomba Sh. milioni 1.5 lakini baadaye akakubali Sh. laki 9.

Baada ya mwizi huyo kunaswa na kukiri kuwa aliiba hela hizo na hata kukubali kutoa faini, mganga huyo alifanya tambiko kuharibi urogi aliofanya awali. 

La kushangaza ni kuwa jamaa huyo alipatikana amefariki keshowe kama ilivyothibitishwa na naibu kamishna wa eneo hilo Jack Obuo.
Na Jackline Mobeyo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA APATWA APATWA NA MAKUBWA BAADA YA KUIBA PESA YA RAMBI RAMBI JAMAA APATWA APATWA NA MAKUBWA BAADA YA KUIBA PESA YA RAMBI RAMBI Reviewed by By News Reporter on 1/24/2019 05:22:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.