Loading...

KILIMO SHADIDI CHALETA MATUMAINI MAPYA

Loading...
Zanzibar. Wakulima wa mpunga wa kilimo cha majaribio cha shadidi, wameongeza uzalishaji kutoka tani 4.3 msimu wa vuli hadi tani 13.5 msimu wa mwaka, baada ya kupatiwa mafunzo ya kilimo hicho.

Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake Darajani, Ofisa elimu kwa wakulima wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Sada Seif Said, alisema wakulima wa kilimo hicho wa Unguja walivuna tani 7.3 za mpunga na Pemba tani 6.2.

Aliyataja mabonde yanayolimwa kilimo cha shadidi kuwa ni Uzini, Cheju, Bumbwisudi, Kibokwa, Makombeni, Weni, Tibirinzi na Kinyapunzi.

Alisema baada ya wakulima kuongeza uzalishaji wataendelea kuhamasisha wakulima wengine wanaolima mpunga wa umwagiliaji maji ili waweze kujiunga na kilimo hicho.

Alielezea matarajio yake kuwa iwapo wakulima watakubali kujiunga kwa wingi na kilimo hicho, Zanzibar inaweza kupunguza kwa asilimia kubwa uagizaji mchele.

Alisema kilimo cha shadidi, kinacholimwa kwa vipindi viwili kwa mwaka, kilianza 2016 na wakulima 85 waliopatiwa mafunzo wanaendelea kulima kwa mafaniko.

“Tutoa elimu kwa wakulima kwa lengo la kukiimarisha zaidi na tumeanza kupata mafanikio,” alisema.

Alieleza wakulima wanatumia mbegu na maji kidogo na kilimo hicho kina uwezo wa kutoa polo 60 za mpunga kwa eka moja wakati kilimo cha kawaida kinazalisha polo 32.

Aliongeza kuwa, kilimo cha shadidi kinachuka muda mfupi zaidi kuanzia wakati wa kupanda, ukuaji hadi kufikia kuvuna tofauti na kilimo cha mpunga wa kawaida.

Aidha alieleza kuwa tayari wizara imeshatoa mafunzo ya kilimo cha hicho kwa Jeshi la Kujenga Uchumi  Upenja ili kukiendeleza.
Na Zaida Msafiri.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KILIMO SHADIDI CHALETA MATUMAINI MAPYA KILIMO SHADIDI CHALETA MATUMAINI MAPYA Reviewed by By News Reporter on 1/09/2019 09:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.