Loading...

WAZIRI SHONZA ATUMIA KAULI YA JPM KUWAONYA GIGY NA WENZAKE, JUU YA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI

Loading...
Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kuporomosha maadili hapa nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Mh. Shonza ameitumia kauli hiyo iliyotolewa na Rais asubuhi jana wakati wa makabidhiano ya kifaa kitakachotumika katika mawasiliano ambacho TCRA wamekabidhiwa ambapo Rais alisema katika moja ya kauli wakati anaelezea madhara ya mitandao ya kijamii na kusema kuwa "Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili"

Baada ya kauli hiyo Mhe. Shonza ambaye ni Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, yaani Naibu anayeshughulikia mambo yaote yanayohusu habari na mawasiliano ameipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema "Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_ogna wenzio,msidhani hatuwaoni , " ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa"
Na Hamisi Bakari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZIRI SHONZA ATUMIA KAULI YA JPM KUWAONYA GIGY NA WENZAKE, JUU YA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI WAZIRI SHONZA ATUMIA KAULI YA JPM KUWAONYA GIGY NA WENZAKE, JUU YA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI Reviewed by By News Reporter on 1/19/2019 11:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.