Loading...
Indonesia. MWANAMKE mmoja ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma moto mumuwe kwa sababu alikataa kumpatia neno siri (password) ya simu yake.
Ilham Cahyani, 25, alimtaka Dedi Purnama, 26, ampatie nenosiri ya simu yake wakati akifanya kazi juu ya dari akitengeneza tailizi katika kijiji cha Pandanwangi, Indonesia, lakini aligoma. Malumbano yalizidi na kuamua kushuka juu ya dari na kuanza kumpiga mkewe huyo.
Hii ilisababisha mapigano ya kimwili na Cahyani alishutumiwa kuchukua mafuta ya petroli kwenye sufuria na kummwagia Dedi. Na baadaye kumchoma kwa kiberiti.
Shuhuda aliyejulikana kama Oji alimsimulia mwandishi wa habari jinsi mwanaume huyo alivyokimbia baada ya kuchomwa na mafuta hayo. Alimuona Dedi anawaka moto na alimsaidia kuzima moto ule.
Kamanda wa polisi Made Yogi alisema Purnama alikimbizwa katika hospitali ya Keruak ili kupata matibabu kwa siku mbili. Bahati mbaya, alifariki baada ya siku ya pili.
Cahyani amekamatwa na jeshi kwa tuhuma za kumuua mumewe na inaripotiwa bado yupo kizuizini katika kituo cha polisi cha Lombok Mashariki.
Na Yuan Busigali.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MKE AMCHOMA MOTO MUWEWE KISA 'PASSWORD' YA SIMU
Reviewed by By News Reporter
on
1/19/2019 12:20:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: