Loading...
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetoa tamko la kulaani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoendelea kujitokeza nchini, likiwamo tukio la mwalimu anayetuhumiwa kumfungia mtoto kabatini.
Tamko hilo lililotolewa jana kwa vyombo vya habari, limekemea vitendo vya ukatili wa watoto majumbani ambavyo vinafanywa na kuhusisha ndugu na walezi wa karibu wa watoto na kuathiri malezi na makuzi ya awali ya watoto kwa kutozingatia haki zao za msingi.
Taarifa ya tamko la wizara hiyo ilisema: "Mapema wiki hii, imeripotiwa mwalimu wa shule ya msingi jijini Dodoma (jina limehifadhiwa) anayetuhumiwa kumfungia mtoto mdogo ndani ya kabati kwa kipindi kirefu na kusababisha afya ya mtoto huyo kudhoofika. Mwalimu huyo anatuhumiwa pia kumfanyia vitendo vya ukatili mama mzazi wa mtoto huyo kwa kumpiga na kumsababishia maumivu mwilini yaliyosababisha binti huyo na mtoto wake kulazwa."
Wizara hiyo imewapongeza wanajamii wote walioibua tukio hilo na kuwezesha Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya uchunguzi, ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Pia, "Katika kipindi hiki ambapo uchunguzi unaendelea kufanyika tunaomba pawe na utulivu na uvumilivu, ili kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa makini na sheria iweze kuchukua mkondo wake," ilisema taarifa hiyo.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

KUFUATIA MTOTO KUFUNGIWA KABATINI, WIZARA YATOA TAMKO HILI
Reviewed by By News Reporter
on
1/03/2019 08:58:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: