Loading...

MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI GHANA, MAELFU WAYAKIMBIA MAKAZI

Loading...
Mapigano kikabila yaliyodumu kwa muda wa wiki moja  mpaka hivi sasa, yaliyojiri kaskazini mwa nchi ya Ghana yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao. 

Kiongozi wa  eneo la kaskazini wa taasisi inayosimamia  majanga ya kitaifa (NADMO) Alhaji Abdullah Hindu, amesema katika eneo la Chereponi makabila ya Konkomba na Chokosi yameingia kwenye mgogoro uliopelekea mapigano.

Hindu alifahamisha kwamba mapigano hayo yaliyoanza Desemba 31 mpaka hivi sasa yamesababisha zaidi ya watu elfu 5 kuyahama makazi yao kwa sababu za kiusalama, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Hindu anaendelea kueleza kwamba katika mapigano hayo mamia ya watu wamejeruhiwa  na nyumba nyingi zimechomwa moto.

Hindu ameelezea kwamba vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo, na hivi sasa ni marufuku mtu yeyote kutoka nje.

Ugomvi kati ya makabila ya Konkomba na Chokosi ulianza mwezi Mei mwaka 2018, baada ya kabila la Kokomba kudai kwamba kipande kimoja cha ardhi ni mali yao. Baada ya viongozi wa makabila hayo kuingilia kati iliamuliwa kwamba mmiliki hali wa ardhi hiyo ni kabila la Chokosi.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI GHANA, MAELFU WAYAKIMBIA MAKAZI MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI GHANA, MAELFU WAYAKIMBIA MAKAZI Reviewed by By News Reporter on 1/08/2019 08:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.