Loading...

WANAJESHI WALIOJARIBU KUMPINDUA RAIS BONGO WATIWA MBARONI

Loading...
Msemaji wa serikali na waziri wa mawasiliano wa Gabon afahamisha kukamatwa kwa wanajeshi waliojaribu kupindua serikali.

Guy-Bertrand Mapangou, waziri wa mawasiliano na msemaji wa  ikulu wa Gabon afahamisha kwamba wanajeshi waliojaribu kupindua serikali na kutangaza katika kituo cha taifa cha redio wametiwa mbaroni.

Waziri huyo wa mawasiliano wa Gabon ameyasema hayo katika  kituo kimoja cha habari cha Ufaransa kwa kuthibitisha kuwa wanajeshi hao  wametiwa mbaroni na kikosi cha GIGN baada ya kuendesha operesheni ya kuokoa kituo cha redio cha  taifa kilichokuwa kimetekwa na wanajeshi hao waliotajwa kuwa wameasi mapema Jumatatu.

Hali imerejea kuwa shwari baada ya muda mchache baada ya makabiliano alifahamisha waziri wa  mawasiliano.

Wanajeshi walioasi walitangaza  katika kituo cha redio cha taifa kuwa wanataraji kulifanyia marekebisho baraza la kitaifa.

Tangazo lililosomwa na   Ondo Obiang Kelly liligonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari huku na kule ulimwenguni.

Jarida la Gabonactu limesema kuwa kulisikika milio ya risasi  mjini Libreville karibu na kituo cha redio ya taifa.

Taarifa zinafahamisha kuwa muda mchache baada ya  wanajeshi walioasi kutangaza kupindua serikali , kituo hicho cha redio kilipoteza mawasiliano na mitandao ya  kijamii kufungwa.

Habari kutoka ikulu zinasema kuwa maeneo yote ya kimkakati nchini Gabon yapo chini ya milki ya serikali.

Ikumbukwe kuwa rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba  alipatwa na maradhi ya ghafla akiwa nchini Saudia Oktoba 24 na kusafirishwa nchini Morocco  Novemba 28.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAJESHI WALIOJARIBU KUMPINDUA RAIS BONGO WATIWA MBARONI WANAJESHI WALIOJARIBU KUMPINDUA RAIS BONGO WATIWA MBARONI Reviewed by By News Reporter on 1/08/2019 08:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.