Loading...

SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WAWAHESHIMU SANA WACHUNGAJI KUZIDI WAUME ZAO

Loading...
WATANZANIA wamechambua kwa nini wanawake huwaheshimu sana wachungaji kuliko wanaume zao, katika maoni kadhaa kupitia njia za mitandao na mahojiano ya ana kwa ana walikuwa na haya ya kuainisha;-

- Wanawake ni rahisi sana kushawishiwa na wachungaji wanalijua hilo.

- Wanawake wanaamini watakutana na wachungaji mbinguni ila wanaume zao wataenda jehanamu (motoni).

- Baadhi ya wanawake huwatazama wachungaji kama watu wenye mamlaka ya kiroho na kuwatazama waume zao kama watu wenye mamlaka ya kimwili tu.

- Mawazo ya wanawake wengi hutekwa na wachungaji, hivyo hudhani yote wanayoambiwa nao ni ukweli, ila wanayoambiwa na waume zao mengine ni ya kupingana nayo.

- Kwakuwa wanaume kuwadharua wake zao huku wachungaji wakiwaheshimu.

- Makanisa mengine ya siku hizi sio sehemu ya ibada tu bali ni sehemu za kufanyia uovu (kama uzinzi) ambapo wale wanawake walioolewa na wale wasioolewa hufanya ukahaba wa kisasa.

- Inategemea kanisa unalosali. Unastahili kutambua kuwa ni Mungu ndiye unayemuabudu na sio mchungaji.

- Wanaamini kuwa wachungaji wanamwakilisha Mungu na kupitia kwao, wanazungumza naye, lakini wachungaji mwishowe kuwanyanyasa kingono badala ya kuwaombea.

- Inategemea utu wa mke na mchungaji wake ni nani.

Na Happyness Mkanyago.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WAWAHESHIMU SANA WACHUNGAJI KUZIDI WAUME ZAO SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WAWAHESHIMU SANA WACHUNGAJI KUZIDI WAUME ZAO Reviewed by By News Reporter on 1/08/2019 07:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.