Loading...

MSANII OMMY DIMPOZ AONEKANA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA UPASUAJI

Loading...
Msanii maarufu wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz ameonekana kwa mara ya kwanza siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Ujerumani.

Msanii huyo aliwashtua mashabiki wake alipotangaza kuwa hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya na kuwa alihitaji matibabu ya dharura.

Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Ommy Dimpoz alisafiri hadi Ujerumani kupata matibabu baada ya kushikwa na tatizo la koo.

Kwa wakati mwingine, kuna uvumi ulioenea kuwa msanii huyo alikuwa ameaga dunia, madai ambayo yalifutiliwa mbali na meneja wake sawa na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ambaye alikuwa akiyafadhili matibabu yake.

Katika chapisho la Instagram lilobainiwa na wanahabari wa Dundiika News, Ommy Dimpoz alionekana akiwa na msanii mwenza Willy Paul.

Kutokana na picha hiyo, ilikuwa wazi kuwa msanii huyo alikuwa amepunguza uzani licha ya hali yake kuonekana kuimarika. 

Dimpoz alisafirishwa hadi Ujerumani kufanyiwa upasuaji wa koo miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji sawa nchini Afrika Kusini.

Baadaye, gavana Joho alimchukua msanii huyo kuishi naye huku hali yake ikiimaarika.

Matatizo ya msanii huyo yalianza katika harusi ya Ali Kiba mjini Mombasa alipobaini kuwa alikuwa na shida ya kumeza chakula.
Na Hamisi Chambo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MSANII OMMY DIMPOZ AONEKANA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA UPASUAJI MSANII OMMY DIMPOZ AONEKANA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA UPASUAJI Reviewed by By News Reporter on 1/22/2019 03:59:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.