Loading...
Watu 11 wapoteza maisha baada ya meli 2 za mizigo kuwaka moto zikipakia mafuta katika bahari nyeusi.
Meli 2 zenye bendera ya Tanzania zilizokuwa zikipakia mafuta katika mlango bahari wa Kerch, nchini Crimea, ya kwanza ililipuka na ndani ya muda mfupi moto ukaenea na kuifikia meli nyingine.
Kati ya mabaharia 31 waliokuwamo kwenye meli hizo 16 ni raia wa Uturuki na 15 ni raia wa India, katika kujiokoa mabaharia hao walijirusha baharini kusubiria msaada.
Urusi ilituma meli za uokoaji kwenye eneo la tukio. Watu 11 walipoteza maisha na wengine 14 waliokolewa. Haijafahamika waliopoteza maisha ni raia wa nchi gani. Kazi ya uokoaji na utafutaji inaendelea, uchunguzi juu ya chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MELI 2 ZA MAFUTA ZENYE BENDERA YA TANZANIA ZAWAKA MOTO MLANGO BAHARI WA KERCH
Reviewed by By News Reporter
on
1/22/2019 10:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: