Loading...
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia raia wa Nigeria anayedaiwa kutapeli Sh. milioni 120 za mafao ya mstaafu nchini.
Utapeli huo ulifichuliwa jana na Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, alipozungumza na waandishi wa habari jijini kutoa tathmini ya mambo mbalimbali yaliyofanywa na jeshi hilo miezi 12 ya mwaka jana.
Kamanda Mambosasa alisema kumekuwapo na wimbi kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini na wamekuwa wanawatesa wakazi wa Dar es Salaam kwa utapeli.
Kamanda Mambosasa aliongeza: "Wako hapa mjini na hawana vitambulisho vya kuingia nchini na wanaendelea kufanya uhalifu wa kuwatapeli wananchi wanaoishi hapa jijini.
"Wananchi wanaumizwa kweli, unakuta mtu anatoka kuchukua kiinua mgongo amestaafu, lakini zinaishia kwa Mnigeria, mmoja hapo chini ametapeli Sh. milioni 120 za mstaafu, lakini ameingia nchini anaishi hapa na hana chochote kinachohalalisha kuwapo nchini."
Kamanda Mambosasa alitoa wito kwa wadau wote wanaohusika na wahamiaji hao ikiwamo Idara ya Uhamiaji, ili kutupia macho zaidi kwa kuwa kuna wimbi la wahalifu wanaingia nchini bila utaratibu na kusumbua wananchi katika taifa letu lenye amani na upendo.
Na Yusuf Mvumbo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

RAIA WA NIGERIA AMTAPELI MSTAAFU MIL. 120/-
Reviewed by By News Reporter
on
1/01/2019 09:08:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: