Loading...

SABABU YA AL SHABAB KUSHAMBULIA KENYA MARA KWA MARA

Loading...
Kenya mara nyingi inashambuliwa na wapiganaji wa al-Shabaab kwa sababu ina mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na ina nguvu ya kiuchumi na hivyo ni rahisi kwa mataifa mengi kutambua shambulizi lolote linalotokea nchini humo.

Wataalamu wamezungumza hayo na kituo cha habari cha Anadolu.

"Kenya ina ujumbe wa kigeni wa kidiplomasia na ni tajiri zaidi katika kanda, hivyo shambulizi lolote linachukua nafasi kubwa sana ulimwenguni ,"Yusuf Serunkuma, mtaafiti katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, amekiambia kituo cha habari cha Anadolu  katika mahojiano siku ya Jumatatu.

Aidha alieendelea kwa kusema kuwa Kenya ina mashirika mengi ya habari na waandishi wa habari wengi wa kigeni mjini Nairobi hivyo mashambulizi hutangazwa sana katika vyombo vya habari ,jambo linalowasaidia magaidi wa Al Shabab kusambaza na  kueneza propaganda zao.

"Mashambulizi ya mara kwa mara nchini Kenya pia yanathibitisha kwamba al-Shabaab bado wana uwezo wa kupigana nje ya mipaka ya Somalia," alisema.

Kikundi cha kigaidi cha al-Qaeda kinachohusishwa na Somalia kimesema hapo awali kuwa mashambulizi hayo hufanyika kwa lengo la kulipiza kisasi uwepo wa majeshi ya kulinda amani ya Kenya nchini Somalia.

Kenya awali ilipeleka askari wake Somalia mnamo Oktoba 2011 baada ya magaidi wa al-Shabaab kuteka wafanyakazi wa kutoa misaada nchini. Lakini baadaye Kenya iliamua  kuchangia askari wake wa kulinda amani katika Umoja wa Afrika (AMISOM)  ili kusaidia kuleta amani kwa jirani yake kaskazini.

Hata hivyo, tangu wakati huo Kenya imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kadhaa, ikiwa ni pamoja na shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa 2015 ambapo watu 148 walipoteza maisha.

Shambulizi la Westgate mjini Nairobi lilisababisha vifo vya watu kadhaa mwaka 2013. Magaidi walitumia mabomu katika mashambulizi hayo.

Mnamo mwaka 2010, al-Shabaab walishambulia maeneo mawili katika mji mkuu wa Uganda wa Kampala na kuua watu kadhaa lakini kwa sasa magaidi hao wameonekana kuhamishia mashambulizi yao nchini Kenya.

Kikundi hicho kwa sasa kimeonekana kuwa na ajenda za kimataifa.

Juma lililopita, al-Shabaab walifanya uhalifu mwingine mkubwa uliosababisha vifo vya watu wengi baada ya kushambulia hoteli moja huko Nairobi.

Watu 21 walipoteza maisha katika shambulizi hilo la kinyama.

Kwa mujibu wa habari,shambulizi hilo lilifanyika kama njia ya kujibu uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutangaza mji wa Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.

Al-Shabaab imekuwa ikipigana na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa ikiwa na matumaini ya kuipindua serikali hiyo ili kuwezesha toleo kali la sheria ya Kiislamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, askari wa amani wa Umoja wa Afrika na Jeshi la Somalia wameweza kupunguza mashambulizi ya kigaidi katika miji mikubwa ukilinganisha na maeneo ya vijijini.

Al-Shabaab pia hufanya mashambulizi ya bomu mara kwa mara nchini Somalia na mashambulizi mabaya zaidi yalitokea  Oktoba 2017 ambapo watu zaidi ya 500 walifariki mjini Mogadishu. Kundi hili mara nyingi hushambulia migahawa na hoteli kwa kutumia mabomu ya gari.

Mbinu hizo hutumika pia wakati wa kuishambulia Kenya.
Na Maulid Masamaki.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SABABU YA AL SHABAB KUSHAMBULIA KENYA MARA KWA MARA SABABU YA AL SHABAB KUSHAMBULIA KENYA MARA KWA MARA Reviewed by By News Reporter on 1/24/2019 06:28:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.