Loading...

SAFARI ZA NDEGE ZA MOJA KWA MOJA KATI YA RWANDA NA ISRAEL KUANZISHWA

Loading...
Rwanda inatarajia kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kuelekea nchini Israel.

Kwa mujibu wa gazeti la Israel la Yedioth Ahronoth, tangazo hilo limekuja baada ya mkutano kati ya waziri wa uchukuzi wa Israel Yisrael Katz na balozi wa Rwanda nchini Israel Joseph Rutabana.

Kulingana na makubaliano yaliyofanywa,Israel na Rwanda zitakuwa na safari saba za ndege kila siku kati ya uwanja wa ndege wa Ben Gurion wa Israel na uwanja wa ndege wa Kigali.

Rutabana amesema kuwa safari hizo zitaanza ndani ya miezi kadhaa ijayo.

Mnamo mwaka 2017,Israel ilifungua ubalozi wake kwa mara ya kwanza nchini Rwanda.
Na Frank Kavikule.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAFARI ZA NDEGE ZA MOJA KWA MOJA KATI YA RWANDA NA ISRAEL KUANZISHWA SAFARI ZA NDEGE ZA MOJA KWA MOJA KATI YA RWANDA NA ISRAEL KUANZISHWA Reviewed by By News Reporter on 1/09/2019 08:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.