Loading...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO HAYA KATIKA WIZARA, AFUNGUA UBALOZI MPYA

Loading...
Rais John Magufuli jana Jumanne ametangaza viongozi mbalimbali aliowateua wakiwamo mawaziri na makatibu wakuu.

Akitangaza mabadiliko hayo jana Jumanne Januari 8, 2019, Ikulu Dar es Salaam Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kusimamia Uwekezaji.

Balozi Kijazi amesema nafasi ya Kairuki imechukuliwa na Dotto Biteko aliyepandishwa kutoka naibu waziri wa wizara hiyo na atashirikiana na naibu wake Stanslaus Nyongo.

Viongozi wengine waliteuliwa ni Joseph Nyamhunga kuwa katibu mkuu Tamisemi akichukua nafasi ya Mussa Iyombe aliyestaafu kwa mujibu wa sheria, na nafasi ya Nyamhanga imechukuliwa na mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Elius Mwakalinga kuwa katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi.

Pia, JPM amemteua Dk Zainab Chaula kuwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya, akichukua nafasi ya Dk Mpoki Ulisubsya aliyeteuliwa kuwa balozi ambaye kituo chake cha kazi kitatangazwa baadaye.

Rais Magufuli amemteua Dk Doroth Mwaluko aliyekuwa naibu katibu ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala bora) kuwa katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, na Profesa Faustine Kamuzora aliteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa wa Kagera kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Athuman Diwani ambaye aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Rais Magufuli amefanya uamuzi wa kufungua ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba na balozi atakayeteuliwa kwenda kituo hicho atatangazwa baadaye.
Na Saidi Bakari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO HAYA KATIKA WIZARA, AFUNGUA UBALOZI MPYA RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO HAYA KATIKA WIZARA, AFUNGUA UBALOZI MPYA Reviewed by By News Reporter on 1/09/2019 08:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.