Loading...
Uganda inadaiwa kiasi cha asilimia 41 ya pato jumla la taifa. Deni la taifa la Uganda limeanza kuwatia wasiwasi Waganda wengi wakihofia kuwa hali hii itazidi kuzorotesha ukuaji wa uchumi wa nchi.
Lakini wadadisi wa masuala ya madeni na uchumi wa nchini humo wana mashaka kama taifa litakuwa na uwezo wa kukidhi mzigo huo mkubwa wa medeni unaongezeka kila kukicha. China ndiyo inaongoza katika kuidai Uganda kiasi kikubwa na kuna hofu kuwa huenda nchi hiyo itatwaa mali za Uganda ili kujilipa deni lake.
Lakini waziri wa fedha Matia Kasaija anakanusha vikali uwezekano wa hatua kama hii kuchukuliwa akisisitiza kuwa Uganda ina uwezo wa kuyalipa madeni yake kwa mujibu wa mikataba iliyosaini.
Mara kwa mara serikali ya Uganda husaini mikataba ya mikopo na mataifa na mashirika mbalimbali ya kigeni kwa ajili ya kile kinachotaja kuwa ujenzi wa miundombinu kuchapua maendeleo ya kiuchumi, kijamii na usalama wa nchi. Miongoni mwa hayo ni barabara na madaraja, mabwawa ya kuzalisha umeme na kadhalika. Serikali inasema kuwepo kwa miundombinu hii japo inatokana na mikopo, ni hatua muhimu katika kubuni nafasi za kazi pamoja na kuvutia wawekezaji wa kigeni.
Pia, mdau wa mswala ya uchumi na mtaalamu wa bajeti Julius Mukunda wa shirika la CSBAG ametahadharisha Waganda kuwa wasichangamkie kuongezeka kwa bajeti ya nchi ya mwaka ujao wa kifedha kwani hadi asilimia 40 ya fedhaa kwenye bajeti hiyo zitatumiwa kulipa madeni pamoja na riba.
Na Yohana John.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MADENI MAKUBWA YA UGANDA YAWAPA RAIA PRESHA
Reviewed by By News Reporter
on
1/09/2019 08:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: