Loading...
Njombe. Watoto watatu kati ya 10 waliotekwa na kukutwa wakiwa wamechinjwa wilayani Njombe ni wa familia moja.
Watoto hao; Godliva Mwenda (11), Gasper Nziku (8) na Giliad Nziku (5) wote wa Danford Nziku walichukuliwa na mtu ambaye hajafahamika walipokuwa wakicheza nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa ambako walichinjwa kisha kunyofolewa viungo vya mwilini.
Walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikando. Godliva alikuwa darasa la nne, Gasper la kwanza na Giliad alikuwa darasa la awali.
Charles Mlonganile, akisoma historia ya marehemu hao kwa niaba ya familia ya Nziku katika mazishi yao yaliyofanyika jana, alisema watoto hao walichukuliwa na mtu nyumbani kwao saa moja jioni Januari 20. Alisema wakati wakichukuliwa, walikuwa watano wote wakicheza nje ya nyumba yao.
“Walibaki watoto wawili hapa nyumbani na walipoulizwa wenzao wako wapi, walisema wamechukuliwa na Joely Nziku,” alisema.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Rashid Ngonyani alisema wanamshikilia Joely, mkazi wa Makambako ambaye ni ndugu wa baba wa watoto hao kwa mahojiano.
Alisema baada ya hapo jitihada za kuwatafuta zilianza kwa ndugu, wananchi na Serikali kupitia Polisi na juzi walipata taarifa kwamba kuna watoto wamepatikana wakiwa wamefariki na ndugu walipokwenda polisi waliwatambua.
Jeshi la Polisi limetaarifu kuwa, baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa na vyombo vya dola vinaendelea kudhibiti na kushughulika na mtandao wa wauaji hao wa raia wasiokuwa na hatia wakiwamo watoto.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WATOTO SITA WAUAWA KINYAMA, WATATU WAKIWA FAMILIA MOJA
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2019 10:12:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: