Loading...
Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu amesema taarifa za kuwa amepigwa na mchumba wake hataki kuzizungumzia kwa kuwa anaona zinalenga kumtoa katika njia yake anayotaka kwenda kwa sasa.
Akizungumza leo Januari 29 katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio E FM, amesema habari hizo zilianza kuenea baada ya kutangaza kampeni yake ya Save my Valentine wiki iliyopita.
"Kama umeshawahi kutazama filamu za mapigano mwishoni utaona adui anavyojaribu kufanya vitu vya kumhadaa starring, hivyo ndivyo nilivyochukulia maneno haya," amesema.
Ameongeza kuwa utakapofika wakati sahihi atalizungumzia hilo na kwamba kwa wakati huu angependa kuendelea na kampeni yake ya kusaidia wasiojiweza.
Akizungumzia kampeni hiyo ya kusaidia wenye uhitaji amesema itaendeshwa kwa fedha anazopata katika mauzo ya nguo zake lakini amewaomba watu binafsi na mashirika wanaotaka kushirikiana naye wajitokeze.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

LULU APOTEZEA KUZUNGUMZIA KICHAPO, KUTOVAA PETE YA UCHUMBA
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2019 10:27:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: