Loading...
Kenya. MWANAMKE mmoja kutoka Pokot Magharibi aliyedaiwa kufariki na baadaye kufufuliwa na Nabii David Owuor wa kanisa la Holiness and Repantance ameaga dunia tena.
Rosa Chapochesau aliyejulikana na wengi kama Mama Rosa alifariki Jumatano, Januari 22, akiwa na umri wa miaka 59 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Baada ya kifo chake, Rosa anadaiwa kuzikwa kisiri siri nyumbani kwake katika kijiji cha Cheparten, Lenan Pokot Kusini.
Kulingana na wenyeji wa Cheparten, kulikuwa na uvumi kuhusu kifo cha Mama Rosa lakini hakuna muunini yeyote wa Kanisa la Owuor aliyezungumza kuhusu habari za mwanamke huyo aliyedaiwa kufufuka 2017.
"Nam amefariki. Tunaambiwa kuwa alipelekwa mjini Eldoret kuishi na daktari aliyetaka kujua kuhusu historia ya afya yake. Tangu wakati huo hatujamuona tena hadi habari kuhusu kifo chake zilipotokea Jumatano," mwenyeji mmoja aliyeomba jina lake lisitajwe.
Licha ya Mama Rosa kuthibitishwa kuugua ugonjwa wa Artheritis, madai mengine yaliibuka kuwa alikuwa akiugua maradhi ya kifafa.
Habari kuhusu kufufuka kwake zilipobainika, mamia ya wenyeji walifika nyumbani kwake kushuhudia muujiza huo.
Baada ya kudaiwa kufufuka, Mama Rosa alihamishwa hadi Eldoret kwa daktari Kasepoi aliyesisitiza alitaka kufuatilia historia ya maradhi yake.
Mama Rosa hakurudi tena nyumbani kwake, wengi wakishangazwa na habari kuhusu kifo chake.
Jarida la TUKO la nchini humo liling'amua kwa mwanamke huyo alizikwa kisisiri na kanisa la Owuor wengi wakiibua masuali kadhaa kulihusu kanisa hilo.
Na Ummy Zakaria.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

AFARIKI TENA BAADA YA KUDAIWA ALIFUFULIWA MIAKA 2 ILIYOPITA
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2019 11:01:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: