Loading...

MAANDAMANO YAENDELEA KUPAMBA MOTO NCHINI SUDAN

Loading...
Mashirika ya wafanyakazi, makundi ya wapinzani  kwa ushirikiano nchini Sudan watoa wito wa maandamano.

Katika taarifa iliyotolewa na viongozi wa wapinzani na mshirika ya wafanyakazi imefahamisha kuwa maandamano yatafanyika katika miji tofauti nchini Sudan Jumanne.

Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji katika jamii. Maandamano hayo yanafanyika nchini Sudan tangu Disemba 19.

Maandamano hayo yalibadilisha sura yake na kuwa maandamano ya kupinga  serikali ya  rais Omar Al Bashir  na kumtaka kuondoka madarakati.

Jeshi la Polisi lilitumia mabomu ya kusabisha kutokwa na machazi kuwatawanya waandamanaji.

Shirika la Amnesty International  limesema kuwa watu 40 ndio waliofariki kufuatia maandamano hayo nchini Sudan.
Na Janeth Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAANDAMANO YAENDELEA KUPAMBA MOTO NCHINI SUDAN MAANDAMANO YAENDELEA KUPAMBA MOTO NCHINI SUDAN Reviewed by By News Reporter on 1/29/2019 11:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.