Loading...

ZARI ATOA POVU KWA WANAOPONDEA MAVAZI YAKE

Loading...
Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka na kuwamwagia Povu zito watu waliomponda Baada ya kuposti picha ya utata.

Siku chache zilizopita Zari aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram zilizomuonyesha akiwa amevaa mavazi ya ndani ‘Swimming costume’ na kupelekea watu kumrushia maneno.

Mashabiki walimjia juu Zari na kumtuhumu kwa picha za nusu uchi na kuanika kwenye mitandao ya kijamii ilhali akiwa ni mama  wa watoto watano na huku watoto wengine wakiwa wakubwa kabisa.

Baada yapovu hilo la mashabiki Zari aliibuka na kuposti kipande cha video kujibu mashambulizi na kwa sababu asilimia kubwa waliokuwa wakimchamba ni Wabongo, akaona naye bora awachambe kwa Lugha ya Kishwahili.

Alisema: "Jamani nikitaka kuvaa swimming cost kwa swim­ming pool hiyo ni maisha yangu, ukitaka kuvaa dera hiyo ni maisha yako usini­pangie maisha vile mimi sikupangii maisha naomba tuheshimiane, samahani".

Zari alivaa mavazi hayo pembezoni mwa bwawa la kuogelea ambapo Hivi sasa yupo nchini Uganda na familia yake.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZARI ATOA POVU KWA WANAOPONDEA MAVAZI YAKE ZARI ATOA POVU KWA WANAOPONDEA MAVAZI YAKE Reviewed by By News Reporter on 1/03/2019 01:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.