Loading...
Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho siku ya Jumatatu, Didemba 31 kwenye mkesha wa mwaka mpya alithibitisha urafiki wake wa dhati kwa msanii wa hapa nchini anayefanya vizuri katika muziki wa bongo fleva Alikiba baada ya kumsaidia kumjazia mashabiki uwanjani baada ya shoo hiyo kuhudhuriwa na watu wachache.
Baada ya mashabiki wachache kuhudhuria katika tamasha hilo lililoandaliwa katika uwanja wa Mombasa Sport Club, Joho aliwaagiza watu kuingia kwenye tamasha hilo bure kwa sharti la kuonyesha vitambulisho.
Ikiwa tamasha hilo liliandaliwa kwa lengo la kuwaburudisha wakazi wa mombasa huku wakisubiri kuukaribisha mwaka mpya, watu wakawaida walipaswa kulipa kiingilio cha Sh. 20,000.
Tamasha hilo likihudhuriwa na watu maarufu kama Kakayake Joho, Abu Joho, mwakilishi wa wanawake Mombasa Aisha Mohamed na spika wa bunge kaunti ya Mombasa Harub Khatri miongoni mwa maafisa wengine wakuu wa kaunti hiyo.
Baadaye, Sauti Sol walijumuika na AliKiba kuwatumbuiza mashabiki usiku kucha.

Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ALIKIBA MANUSURA ALAMBE GARASA SHOO YA MOMBASA, GAVANA AMSAIDIA
Reviewed by By News Reporter
on
1/03/2019 12:57:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: